HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI KUPUNGUZA TATIZO LA WALIMU WA SAYANSI.
Halmashauri ya wilaya ya masasi
itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza
kufeli kwa masomo ya sayansi katika shule za sekondari baada ya kupata walimu 45 kati ya 74 waliopangwa ni wa masomo
ya sayansi huku masomo ya sanaa yakiwa na walimu 27 tu.
Akizungumza wakati wa kuwapokea walimu hao mei 2015 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri a wilaya
ya masasi bibi Beatrice R Dominic aliishukuru serikali kwa kuwaleta walimu
wengi wa masomo ya sayansi, hali itakayosaidia wanafunzi kujifunza masomo ya
sayansi kwa ubora.
“walimu wa masomo ya yasansi
waliopangwa katika halmashuri ya wilaya
ya masasi wamepangiwa vituo yaani shule za kufundisha kutoka serikali kuu ili
wasilalamike au kukataa vituo hasa vilivyopo kijijini” alisema Beatrice
Aidha, mpaka tarehe ya mwisho ya
kuripoti ni walimu 57 sawa na asilimia
77% wakiwemo wanaume 48 na wanawake 9 tu
ndio walioripoti kati yao walimu wa
masomo ya sayansi 30 na sanaa 27.